1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican: Papa Francis hatohudhuria mkutano wa COP28

29 Novemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ameifuta safari yake ya kwenda kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28, utakaoanza wiki hii mjini Dubai kutokana na maradhi.

https://p.dw.com/p/4ZYdS
Vatikanstadt 2023 | Papst Franziskus bei der wöchentlichen Generalaudienz
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.Picha: Riccardo De Luca/UPDATE IMAGES PRESS/MAXPPP/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa na msemaji wa makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican, Matteo Bruni, alipozungumza na waandishi habari jana jioni.

Afisa huyo amesema licha ya kuimarika kwa hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa kiroho, Baba Mtakatifu Francis hatoweza kufanya ziara yake ya siku tatu huko Umoja wa Falme za Kiarabu kutokana na ushauri wa madaktari.

Papa Francis alipata maambukizi ya mafua na uvimbe kwenye mapafu mwishoni mwa juma.

Wiki hii alikuwa amepangiwa kuhudhuria mkutano wa COP28 na kuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki kutoa hotuba mbele ya kongamano hilo la mazingira linalotafuta njia za kulishughulikia janga la mabadiliko ya hali ya hewa.