1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNAIDS inamatumaini yakumaliza UKIMWI ifikapo 2030

28 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa inawezekena kuumaliza kabisa ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030, iwapo tu mashirika ya kijamii mashinani na watu walioko katika mstari wa mbele kupambana na ugonjwa huo watawezeshwa.

https://p.dw.com/p/4ZY4g
Kanada World AIDS Conference
Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIS Winnie Byanyima katikati akiongoza mjadala wa kumaliza UKIMWI duniani.Picha: THE CANADIAN PRESS/Ryan Remiorz/empics/picture alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi UNAIDS, limesema katika ripoti yake ya kila mwaka ya siku ya Ukimwi duniani kwamba juhudi za mashirika ya kijamii mashinani hazitambuliki, na kwamba zinapewa ufadhili mdogo na hata wakati mwengine watu hao hushambuliwa.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, ingawa dunia bado haijakomesha kabisa ugonjwa wa Ukimwi kama tishio la afya kwa umma, kuna matumaini ya hilo kuafikiwa.

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza uliweka lengo mwaka 2015 la kuutokomeza Ukimwi kama tishio la afya kwa umma ifikapo mwaka 2030.

Soma pia:Tanzania yabadili gia mapambano dhidi ya Ukimwi

Kwa sasa, kuna watu milioni 39 wanaoishi na virusi vya HIV duniani kote, virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi. Kati ya hao, milioni 20.8 wako mashariki na kusini mwa Afrika huku wengine milioni 6.5wakiwa barani Asia na Pasifiki.

Hata hivyo kati ya wagonjwa milioni 39, milioni 9.2 hawana dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.

Hatua yapigwa kuelekea upatikanaji rahisi wa dawa za kufubaza Ukimwi