1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taifa Stars yaangukia pua mbele ya Morocco jijini Dar

22 Novemba 2023

Timu ya taifa ya Morocco imeifunga Tanzania mabao 2-0 katika mchezo wao wa ufunguzi wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2026.

https://p.dw.com/p/4ZHur
Michuano ya Kombe la Dunia la Qatar mwaka 2022 kati ya Morocco na Uhispania
Wachezaji wa timu ya taifa ya MoroccoPicha: Matthew Childs/REUTERS

Mechi hiyo ya kusisimua, ilichezwa katika uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam.

Winga wa Morocco Hakim Ziyech aliifungia timu yake ya Simba wa Atlas kunako dakika ya 28 ya mchezo kabla ya mchezaji wa Tanzania Lusajo Elukanga kujifunga mwenyewe kunako dakika ya 53 na kuihakikisha Morocco ushindi.

Morocco imepangwa katika kundi E pamoja na Zambia, Congo, Taifa Stars Tanzania, Niger na Eritrea.

Michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2026 itafanyika nchini Canada, Marekani na Mexico kati ya Juni 11 na Julai 19.

Shirikisho la soka duniani FIFA limebadilisha mfumo wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026, ambalo litakuwa la kwanza kushirikisha timu 48 badala ya 32.